Jumapili, 19 Aprili 2020

"TUENDELEE KUCHUKUA TAHADHARI" DED LUDEWA

Endelea kujikinga na uwakinge wengine na ugonjwa wa Corona.

Na Mwandishi wetu:
Ludewa.
Wanakwaya wa kwaya ya Parapanda KKKT LUDEWA wameshirikiana na wakristo wote nchini katika kuliombea Taifa letu la Tanzania kuhusiana na janga la CORONA lililoikumba nchi na Dunia kwa ujumla. Hatua hii inakuja mara baada ya agizo la Mhe. Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Joseph Magufuli kuwaomba waumini wote wa dini na madhehebu mbalimbali kuwa na maombi ya mfungo wa siku tatu tangu tar 17-19/4/2020 kwaajili ya ugonjwa huo.

Serikali inasisitiza kuendelea kuchukua TAHADHARI ya kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya ugonjwa huu hatari wa MAPAFU unaosababishwa na virusi vya corona, COVID19.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni