1.
KUZALIWA
Hantish ailzaliwa mnamo tarehe 02/10/1991 katika hospitali
ya kilutheri ya ilembula iliyoko kwenye kata ya ilembula, tarafa ya
wanging’ombe, wilaya ya wanging’ombe na mkoa wa njombe.
2.
FAMILIA ANAYO TOKA
Hantish ni mtoto wa kwanza katika familia ya Mr. Jozack
Mhugo yenye watoto wawili, ambapo mtoto wao
wa pili anaitwa Atukuzwe Mhugo.
Familia hiyo ni wazawa wa kijiji cha usuka, kata ya usuka,
tarafa ya mdandu, wilaya ya wanging’ombe na mkoa wa njombe.
3.
MAKUZI
Akiwa bado na umri mdogo sana hantish alilelewa na wazazi
wake (baba na mama) katika nyumba yao iliyo kuwa kijijini kwao usuka, mtaa wa
kanisani. Akiwa na umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu mama yake alimtoroka na
kuitelekeza familia yake katika hali tete. Kwa kipindi chote cha nyuma mama
yake(Christina mbakilwa) alikuwa
akijihusisha na biashara ya uuzaji wa nyanya. Hivyo alifaulu kutoroka katika
mazingira hayo.
Baada ya mama yake
kutoroka hantish hakuweza kulelewa na baba yake, hivyo alipelekwa na kuishi na
bibi yake (anna haule) aliyeishi mtaa wa itula A, kijijini hapo usuka.
4.
MAISHA YAKE NA BIBI
“jembe halimtupi mwenye mpini” ni maneno ya wahenga hayo. Pamoja na maisha maagumu ya hantish na
bibi yake kwenye nyumba ya makuti lakini Mungu alizidi kmpigania malaika wa Mungu (hantish).
Alizoea kila asubuhi kupata kifungua kinywa cha uporo wa
ugali uliobaki jana, hayo yote alihudumiwa na bibi yake. Pamoja na kuyazoea
maisha ya bibi lakini ilikuwa ni vigumu kuvumilia kuishi karibu na shangazi
yake (Eneza mhugo) kwani ilikuwa kila akiondoka tu bibi yake, hantish alikuwa
akinyanyaswa sana. “nenda kaniletee maji ya kunywa” ni maneno ya shangazi yake
akimtuma hantish wakiwa jirani na moto kwa chakula cha jioni.kwa upole na unyonge
Hantish aliyaleta maji yale kwenya birika ambayo haikuwezekana kujaza maji hadi pomoni kwa kuzuia kumwagika ovyo. “wee
mjinga kweli..kwanini umeleta maji kidogo?” alikaripia shangazi yake huku
akinyanyua kijinga cha moto na kumtupia mdomoni mwake. Hiyo ni miongoni mwa
vitisho vilivyomtokea Hantish pindi alipo baki na shangazi yake mara baada ya
bibi yake kuondoka. Pamoja na hayo Hantish alivumilia.
5.
KABLA YA KUANZA SHULE YA MSINGI
Wakati baba yake akitafuta maisha mapya ya kuishi na mke
mwingine, bahati nzuri jitihada hizo hazikufanikiwa baada ya kufanikiwa kumpata
mama mzazi wa hantish na kumrudisha nyumbani tayari kwa kuishi na mume wake na
wamlee mtoto wao(hantish).
Ilikuwa ni mwaka
1992 ambapo familia hiyo ilibahatika kumpata mtoto wao wa pili aitwaye Atukuzwe
Mhugo. Maono yalionyesha kuwa ndoa iliyo kuwa na misukosuko sasa imesimama
imara , lakini mambo yakawa sivyo ndivyo. Baada ya muda wa miezi 6 toka
ajifungue mtoto wa pili mama hantish alimtoroka tena pamoja na mtoto wa pili
mgongoni.
Baada ya kuishi
hivyo kwa kipindi chote. Baba mzazi wa hantish aliamua kwenda na kuhamia Mbeya
kwa makazi mapya kwa lengo la kuwa mbali kidogo kimaisha. Huko baba huyo
alijihusisha na ufundi cherehani akiwa ni mshonaji mzuri sana wa kofia za
singa. Ndipo alipo bahatika kumpata mke wa kinyakyusa, wakaishi wote kama baba
na mama wa hantish. Kwa muda wote huo
hantish hakuwahi kwenda Mbeya kwani bado alikuwa akiishi na bibi yake
Usuka.
Mwaka 1999 hantish
Akiwa na umri wa miaka 9 ni mwaka utakao kumbukwa kwa matukio ikiwemo msiba wa
Mwl. Nyerere ambapo bibi hantishi
aliugua sana kiasi kilicho pelekea hadi familia ya mzee Godwin Mhugo kuuza
mashamba ili wapate fedha za kwenda Dar-es-salaam kwa matibabu. Hivyo ilibidi
hantish abaki na shangazi yake(Eneza Mhugo) kwa muda wote ambao bibi yake
hatakuwepo. Mambo yalivyo pangwa yakapangika. Hali ikawa si shwari nyumbani
kwani hantish alianza kuishi maisha ya kushurutishwa sana na shangazi yake,
hali iliyo pelekea hata majirani kulitambua hilo na kupeleka taarifa Mbeya kwa
wazazi wa hantish ili waende wamchukue akaishi mbeya pia kwa muda wote hata
atakapoanza elimu ya msingi mwakani.
6.
MAISHA YA SHULE
Mwaka 2000 hantish alianza darasa la kwanza katika shule ya
msingi mwenge iliyopo jijini mbeya. Hakuweza kuendelea na masomo katika shule
ile ambapo baada ya miezi 9 alihitajika kurudi kijijini Usuka kuishi na bibi
yake aliyerudi kutoka matibabuni. Kwa sababu bibi alimhitaji sana mjukuu wake,”nyevaa
mnirudishie mjukuu wangu…” Ni baadhi tu ya maneno yaliyoandikwa katika barua ya
Bibi yake Hantish ikiwataka wazazi wa Hantish wamrudishie bibi yao mjukuu wake
kwa kuwa alikua amemkumbuka sana. wazazi
hawakuwa na usemi juu ya hilo, alirudi hantish kwa bibi yake ambak o ilimlazimu
aanze darasa la kwanza kwa mwaka 2001 januari
7.
A. ELIMU YA MSINGI
Mwaka 2001 januari
hantishi alianza kuipata elimu ya msingi na kuhitimu mwaka 2007 katika shule ya msingi
usuka. Katika kusoma kwake hantish alionekana ni mtoto wa pekee asiye penda
uchafu kitendo kilicho pelekea hata walimu wakamchagua kuwa kiranja wa mazingira.
Hata hivyo alipohitimu alitunukiwa cheti cha usafi.
7 . B. ELIMU YA SEKONDARI
Ilikuwa ni mwaka 2008 januari ambapo hantish alianza elimu
ya sekondari katika shule ya sekondari ya igwachanya iliyopo katika wilaya ya
wanging’ombe ambapo kwa wakati huo ilikuwa ni wilaya ya njombe kabla serikali
haijagawanya maeneo. Kwa wakati wote akiwa masomoni hantish alionekana kuwa ni
mtu mwenye vipaji tofauti na elimu anayo ipata. Miongoni mwa vipaji alivyokywa
navyo ni pamoja na uchoraji, utunzi na uandishi wa mashairi, tenzi, nyimbo,
ngonjera na simulizi(hadithi) mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupiga baadhi ya
vyombo vya muziki kama vile;-kinanda na gita. Vipaji hivyo viliweza kumpatia na
kuipatia sifa shule ya igwachanya ambapo
mwaka 2009 oktoba(Akiwa kidato cha II) hantish aliibuka kuwa mshindi wa tatu
katika shindano la uchoraji wa picha za TAKUKURU(PCCB) ambalo liliwashindanisha
wanafunzi 276 kiwilaya. Mwaka uliofuata
(2010) hantish aliteuliwa kuuwakilisha mkoa wa njombe ki-UKWATA katika kongamano
la ukanda, ukanda wa kusini(zonal conference, southern zone) lililofanyika mkoa
wa Ruvuma(Songea) katika shule ya sekondari ya wavulana –songea(songea boys
school). Na mwaka 2011 akiwa kidato cha
nne aliongoza kundi la UKWATA tawi la Igwachanya katika mashindano ya uimbaji
kwa siku za pasaka ambao ulifanyika katika seinari ya kidugala.
Katika fani ya
uandishi na utunzi wa mashairi na ngonjera ndiyo ilyo wafanya wanaUKWATA tawi
la igwachanya washike nafasi ya saba kati ya kumi na nane kwa alama ya 82%
daraja A.
8.
BAADA YA KUHITIMU ELIMU YA SEKONDARI
Ndoto zake katika
elimu yake ilikuwa ni kuwa daktari siku moja. Alihitimu mafunzo ya elimu ya
sekondari mwaka 2011 akiwa na umri wa miaka 21. Baada ya kuhitimu hantish
aliombwa kwenda kuifundisha shule ya msingi iliyopo katika kijiji cha
isindagosi. Huko alifanikiwa kufundisha masomo ya sayansi na kiingereza. Kwa
wakati huo wote akisubiri matokeo ya mtihani wa kidato cha nne aliweza
kujihusisha na biasha ra ya usambazaji wa mboga na nyanya vijijini, alifanikiwa
kuanzisha darasa la mafunzo ya jioni (tuition) kwa wanafunzi mbalimbali wa
shule ile ya isindagosi, ailombwa pia kuifundisha kwaya ya isharika huo wa
isindagosi kwa muda wote aliokuwepo. Huko alifanikiwa kpata shamba na kulima
mazao(mahindi na maharage). Kwa upande Fulani maisha yake hantish alikuja
kumfaa kwa wakati wote apokuwa akisubiri matikeo
Baada ya matokeo
kutoka yeye alipata daraja la IV.
9.
BAADA YA MATOKEO YA MTIHANI KUTOKA.
Hantish alibahatika kujiunga na chuo cha uuguzi na ukunga
kilichopo jirani na hospitali ya rufaa ya ilembula mwaka 2012 septemba tarehe
25. Aliendelea na masomo na hatimaye alihitimu masomo hayo mmnamo mwaka 2014
August. 25.
Akiwa chuoni hantish
alifahamika kwa kipaji alichokuwa nacho cha uimbaji wa muzicki wa injili,
ikizingatiwa na kuwa mahali pale palikuwa ni chuo cha kidini. Mwaka 2013 mwezi
wa 10 tar.25 kwa mara ya kwanza chuo kumpata mwanamuziki, hantish alifanya
uzinduzi wa wimbo wake wa kwanza ulio itwa ‘NIKUPE NINI MWILI?’ alio
washirikisha wanafunzi wenzake ambao ni:- emilyo msigala na nuru kalengo ambao
nao walisikika kupitia kipaji hicho. Ndipo lilipo undwa kundi moja na kuitwa
‘THE WINNER’S BAND’ yaani kundi la washindi.
Mbali na kuwa mwanamuziki hantishi aliweza kuwa kiongozi
katika ngazi ya mkoa akiiwakilisha wilaya ya kusini magharibi ki-UKWATA kwa
mwaka 2012-13.
10.
BAADA YA KIHITIMU CHUO CHA UUGUZI NA UKUNGA
Ikiwa ni kabla ya matokeo
na vyeti vya wahitimu kutoka ulikuwa ni mwezi wa 9 tar. 2 mwaka 2014
hatua za ajira zlikamilika na hantish akawa ni miongoni mwa waaliajiriwa kwenye
hospitali ya rufaa ya ilembula haitmaye akaanza kazi mara moja.
Pamoja na sanaa aliyo kuwa nayo lakini aliiheshimu sana kazi
yake, alijitahidi kuutmia muda vizuri kwenye kazi huku akiamini kuwa anaweza
kuupata muda wakufanya mazoezi yake binafsi ya muziki.
11.
MAFANIKIO ALIYOYAPATA
“mafanikio ni mengi, siwezi kuyaeleza yote hapa lakini
namshukuru Mungu kwa kunipa kipaji hiki cha uimbaji na taaluma ya uuguzi na
ukunga. Wengi huwa wanasema mshika mawili moja humponyoka, lakini kwangu ni
heri kwani siamini kama nimeweza kwenda na muziki na masomo.” Alisema hantish.
Pia aliongeza kuwa mbali na hayo yote aliyo yapata, ameweza kuandaa albam yenye
nyimbo 8 kwa mchanganuo ufuatao;- 1. Nikupe nini mwili? 2. Asubuhi njema. 3.
Tunakuabudu Bwana. 4. Iguse Tanzania. 5. Nimekukimbilia wewe. 6. Fanya hima
niokoe. 7. Twaja mbele zako. 8. Siku yaja.
ukoo wake hantish kwa upande wa mamayake
babu yake anaitwa Omary Juma mbakilwa, alioa mke wa kwanza
aliyeitwa Bi. Ester Mchechumkulu ambaye alikua ni mtu wa Tanga kutoka katika
kabila la wasambaa. Babu na bibi huyo walibahatika kuwa na mtoto mmoja
aliyeitwa Christina mbakilwa ambaye ndiye aliyekuwa kifungua mimba na kitinda
mimba pekee. Kutoka na mazingira
waliyokua wakiishi, babu aliamua kumwacha bibi ester na kumpata mke mwingine
aliyeitwa Bi. Eliza Nyondo, mtu wa Malawi ambaye awali alitokea makete
ukingani. Bibi huyo alijaliwa kumzalia babu watoto saba. 1. Asia 2. God 3.
Joyce 4. Eliud 5. Anna 6. Agness 7. Alfa.
Lakini kuna watoto
aliobahatika kuwa nao babu kabla hajaingia
katika ndoa, ambao ni:- Jozack na mwezie ambaye alifariki. Daniel na
Kelvin ni watoto aliowalea tangu baba yao ambaye ni mdogo wa omary
mbakilwa{babu} afariki akiwaacha wadogo sana.

kumbe...
JibuFuta