Ijumaa, 29 Januari 2016

SOMO: KUISHI KWA UJASIRI NDANI YA YESU

. Rumi 8:31, Zab 118:6 
Mungu yu upate wetu, kwanini uogope? 
Isaya 41:10 anasisitiza bado na kusema usiogope. hebu utambue kitu kimoja kuwa  ili upate ushindi wa kihistoria ni lazima upambane na mambo ambayo wewe unayaona kuwa ni magumu lakini hayo yote ni ruhusa toka kwa MUNGU. lengo lake ajivunie kuhusu wewe na kwamba wewe ni mwanae bora, kwa lugha nyingine tungeweza kusema wewe ni "kidume" mbele za MUNGU. kwa hiyo achana na mambo mepesi bali pambana n ayale uyaonayo kuwa ni magumu kwako ili ukiyashinda yakutengenezee historia na yakamilishe ushuhuda wako.
Zab 27:1 "Bwana ni nuru yako....utayashinda yakutesayo..." ...MUNGU anasema ukimkabidhi yeye maisha yako atakua adui wa adui zako{kutoka 23:22} aaamen!!!   kwa maombi na maombezi wasiliana nami kwa simu namba:- 0768788303 

Jumamosi, 16 Januari 2016

NIKUPE NINI MWILI? By hantish mhugo

mhugo digital studio present to you Abigael Mlawa

NINAMSHUKU MUNGU KWA YOTE ALIYO NITENDEA.

Ni uhalisia usiokwepeka kwamba kila mmoja ana mengi ya kumweleza Mungu wake kwa mema aliyomtendea. Basi kwa kuwa sisi sote tu mali ya Bwana Mungu, kila mwenye pumzi na amsifu yeye aliye tukuka. huu ni mwaka mwingine wa 2016, weka malengo yako kwa Mungu naye atakuongoza katika kila ulitakalo. barikiwa sana.
niwatakie mafanikio mema katika kazi, biashara na vibarua vyenu. Mungu awabariki sana.

ev. hantish mhugo afunguka historia




1.       KUZALIWA
Hantish ailzaliwa mnamo tarehe 02/10/1991 katika hospitali ya kilutheri ya ilembula iliyoko kwenye kata ya ilembula, tarafa ya wanging’ombe, wilaya ya wanging’ombe na mkoa wa njombe.
2.       FAMILIA ANAYO TOKA
Hantish ni mtoto wa kwanza katika familia ya Mr. Jozack Mhugo yenye watoto wawili, ambapo mtoto wao  wa pili anaitwa Atukuzwe Mhugo.
Familia hiyo ni wazawa wa kijiji cha usuka, kata ya usuka, tarafa ya mdandu, wilaya ya wanging’ombe na mkoa wa njombe.
3.       MAKUZI
Akiwa bado na umri mdogo sana hantish alilelewa na wazazi wake (baba na mama) katika nyumba yao iliyo kuwa kijijini kwao usuka, mtaa wa kanisani. Akiwa na umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu mama yake alimtoroka na kuitelekeza familia yake katika hali tete. Kwa kipindi chote cha nyuma mama yake(Christina mbakilwa)  alikuwa akijihusisha na biashara ya uuzaji wa nyanya. Hivyo alifaulu kutoroka katika mazingira hayo.
    Baada ya mama yake kutoroka hantish hakuweza kulelewa na baba yake, hivyo alipelekwa na kuishi na bibi yake (anna haule) aliyeishi mtaa wa itula A, kijijini hapo usuka.
4.       MAISHA YAKE NA BIBI
“jembe halimtupi mwenye mpini” ni maneno ya wahenga  hayo. Pamoja na maisha maagumu ya hantish na bibi yake kwenye nyumba ya makuti lakini Mungu alizidi kmpigania malaika  wa Mungu (hantish).
Alizoea kila asubuhi kupata kifungua kinywa cha uporo wa ugali uliobaki jana, hayo yote alihudumiwa na bibi yake. Pamoja na kuyazoea maisha ya bibi lakini ilikuwa ni vigumu kuvumilia kuishi karibu na shangazi yake (Eneza mhugo) kwani ilikuwa kila akiondoka tu bibi yake, hantish alikuwa akinyanyaswa sana. “nenda kaniletee maji ya kunywa” ni maneno ya shangazi yake akimtuma hantish wakiwa jirani na moto kwa chakula cha jioni.kwa upole na unyonge Hantish aliyaleta maji yale kwenya birika ambayo haikuwezekana kujaza maji  hadi pomoni kwa kuzuia kumwagika ovyo. “wee mjinga kweli..kwanini umeleta maji kidogo?” alikaripia shangazi yake huku akinyanyua kijinga cha moto na kumtupia mdomoni mwake. Hiyo ni miongoni mwa vitisho vilivyomtokea Hantish pindi alipo baki na shangazi yake mara baada ya bibi yake kuondoka. Pamoja na hayo Hantish alivumilia.
5.       KABLA YA KUANZA SHULE YA MSINGI
Wakati baba yake akitafuta maisha mapya ya kuishi na mke mwingine, bahati nzuri jitihada hizo hazikufanikiwa baada ya kufanikiwa kumpata mama mzazi wa hantish na kumrudisha nyumbani tayari kwa kuishi na mume wake na wamlee mtoto wao(hantish).
  Ilikuwa ni mwaka 1992 ambapo familia hiyo ilibahatika kumpata mtoto wao wa pili aitwaye Atukuzwe Mhugo. Maono yalionyesha kuwa ndoa iliyo kuwa na misukosuko sasa imesimama imara , lakini mambo yakawa sivyo ndivyo. Baada ya muda wa miezi 6 toka ajifungue mtoto wa pili mama hantish alimtoroka tena pamoja na mtoto wa pili mgongoni.
  Baada ya kuishi hivyo kwa kipindi chote. Baba mzazi wa hantish aliamua kwenda na kuhamia Mbeya kwa makazi mapya kwa lengo la kuwa mbali kidogo kimaisha. Huko baba huyo alijihusisha na ufundi cherehani akiwa ni mshonaji mzuri sana wa kofia za singa. Ndipo alipo bahatika kumpata mke wa kinyakyusa, wakaishi wote kama baba na mama wa hantish.  Kwa muda wote huo hantish hakuwahi kwenda Mbeya kwani bado alikuwa akiishi na bibi yake Usuka.  
  Mwaka 1999 hantish Akiwa na umri wa miaka 9 ni mwaka utakao kumbukwa kwa matukio ikiwemo msiba wa Mwl. Nyerere ambapo  bibi hantishi aliugua sana kiasi kilicho pelekea hadi familia ya mzee Godwin Mhugo kuuza mashamba ili wapate fedha za kwenda Dar-es-salaam kwa matibabu. Hivyo ilibidi hantish abaki na shangazi yake(Eneza Mhugo) kwa muda wote ambao bibi yake hatakuwepo. Mambo yalivyo pangwa yakapangika. Hali ikawa si shwari nyumbani kwani hantish alianza kuishi maisha ya kushurutishwa sana na shangazi yake, hali iliyo pelekea hata majirani kulitambua hilo na kupeleka taarifa Mbeya kwa wazazi wa hantish ili waende wamchukue akaishi mbeya pia kwa muda wote hata atakapoanza elimu ya msingi mwakani.
6.       MAISHA YA SHULE
Mwaka 2000 hantish alianza darasa la kwanza katika shule ya msingi mwenge iliyopo jijini mbeya. Hakuweza kuendelea na masomo katika shule ile ambapo baada ya miezi 9 alihitajika kurudi kijijini Usuka kuishi na bibi yake aliyerudi kutoka matibabuni. Kwa sababu bibi alimhitaji sana mjukuu wake,”nyevaa mnirudishie mjukuu wangu…” Ni baadhi tu ya maneno yaliyoandikwa katika barua ya Bibi yake Hantish ikiwataka wazazi wa Hantish wamrudishie bibi yao mjukuu wake kwa kuwa alikua amemkumbuka sana.  wazazi hawakuwa na usemi juu ya hilo, alirudi hantish kwa bibi yake ambak o ilimlazimu aanze darasa la kwanza kwa mwaka 2001 januari
7.       A. ELIMU YA MSINGI
  Mwaka 2001 januari hantishi alianza kuipata elimu ya msingi  na kuhitimu mwaka 2007 katika shule ya msingi usuka. Katika kusoma kwake hantish alionekana ni mtoto wa pekee asiye penda uchafu kitendo kilicho pelekea hata walimu wakamchagua kuwa kiranja wa mazingira.
Hata hivyo alipohitimu alitunukiwa cheti cha usafi.
      7 . B. ELIMU YA SEKONDARI
Ilikuwa ni mwaka 2008 januari ambapo hantish alianza elimu ya sekondari katika shule ya sekondari ya igwachanya iliyopo katika wilaya ya wanging’ombe ambapo kwa wakati huo ilikuwa ni wilaya ya njombe kabla serikali haijagawanya maeneo. Kwa wakati wote akiwa masomoni hantish alionekana kuwa ni mtu mwenye vipaji tofauti na elimu anayo ipata. Miongoni mwa vipaji alivyokywa navyo ni pamoja na uchoraji, utunzi na uandishi wa mashairi, tenzi, nyimbo, ngonjera na simulizi(hadithi) mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupiga baadhi ya vyombo vya muziki kama vile;-kinanda na gita. Vipaji hivyo viliweza kumpatia na kuipatia sifa shule ya igwachanya  ambapo mwaka 2009 oktoba(Akiwa kidato cha II) hantish aliibuka kuwa mshindi wa tatu katika shindano la uchoraji wa picha za TAKUKURU(PCCB) ambalo liliwashindanisha wanafunzi 276 kiwilaya.  Mwaka uliofuata (2010) hantish aliteuliwa kuuwakilisha mkoa wa njombe ki-UKWATA katika kongamano la ukanda, ukanda wa kusini(zonal conference, southern zone) lililofanyika mkoa wa Ruvuma(Songea) katika shule ya sekondari ya wavulana –songea(songea boys school). Na mwaka  2011 akiwa kidato cha nne aliongoza kundi la UKWATA tawi la Igwachanya katika mashindano ya uimbaji kwa siku za pasaka ambao ulifanyika katika seinari ya kidugala.
  Katika fani ya uandishi na utunzi wa mashairi na ngonjera ndiyo ilyo wafanya wanaUKWATA tawi la igwachanya washike nafasi ya saba kati ya kumi na nane kwa alama ya 82% daraja A.
8.       BAADA YA KUHITIMU ELIMU YA SEKONDARI
  Ndoto zake katika elimu yake ilikuwa ni kuwa daktari siku moja. Alihitimu mafunzo ya elimu ya sekondari mwaka 2011 akiwa na umri wa miaka 21. Baada ya kuhitimu hantish aliombwa kwenda kuifundisha shule ya msingi iliyopo katika kijiji cha isindagosi. Huko alifanikiwa kufundisha masomo ya sayansi na kiingereza. Kwa wakati huo wote akisubiri matokeo ya mtihani wa kidato cha nne aliweza kujihusisha na biasha ra ya usambazaji wa mboga na nyanya vijijini, alifanikiwa kuanzisha darasa la mafunzo ya jioni (tuition) kwa wanafunzi mbalimbali wa shule ile ya isindagosi, ailombwa pia kuifundisha kwaya ya isharika huo wa isindagosi kwa muda wote aliokuwepo. Huko alifanikiwa kpata shamba na kulima mazao(mahindi na maharage). Kwa upande Fulani maisha yake hantish alikuja kumfaa kwa wakati wote apokuwa akisubiri matikeo
   
 Baada ya matokeo kutoka yeye alipata daraja la IV.

9.       BAADA YA MATOKEO YA MTIHANI KUTOKA.
Hantish alibahatika kujiunga na chuo cha uuguzi na ukunga kilichopo jirani na hospitali ya rufaa ya ilembula mwaka 2012 septemba tarehe 25. Aliendelea na masomo na hatimaye alihitimu masomo hayo mmnamo mwaka 2014 August. 25.
 Akiwa chuoni hantish alifahamika kwa kipaji alichokuwa nacho cha uimbaji wa muzicki wa injili, ikizingatiwa na kuwa mahali pale palikuwa ni chuo cha kidini. Mwaka 2013 mwezi wa 10 tar.25 kwa mara ya kwanza chuo kumpata mwanamuziki, hantish alifanya uzinduzi wa wimbo wake wa kwanza ulio itwa ‘NIKUPE NINI MWILI?’ alio washirikisha wanafunzi wenzake ambao ni:- emilyo msigala na nuru kalengo ambao nao walisikika kupitia kipaji hicho. Ndipo lilipo undwa kundi moja na kuitwa ‘THE WINNER’S BAND’ yaani kundi la washindi.
Mbali na kuwa mwanamuziki hantishi aliweza kuwa kiongozi katika ngazi ya mkoa akiiwakilisha wilaya ya kusini magharibi ki-UKWATA kwa mwaka 2012-13.
 
10.   BAADA YA KIHITIMU CHUO CHA UUGUZI NA UKUNGA
Ikiwa ni kabla ya matokeo  na vyeti vya wahitimu kutoka ulikuwa ni mwezi wa 9 tar. 2 mwaka 2014 hatua za ajira zlikamilika na hantish akawa ni miongoni mwa waaliajiriwa kwenye hospitali ya rufaa ya ilembula haitmaye akaanza kazi mara moja.
Pamoja na sanaa aliyo kuwa nayo lakini aliiheshimu sana kazi yake, alijitahidi kuutmia muda vizuri kwenye kazi huku akiamini kuwa anaweza kuupata muda wakufanya mazoezi yake binafsi ya muziki.

11.   MAFANIKIO ALIYOYAPATA
“mafanikio ni mengi, siwezi kuyaeleza yote hapa lakini namshukuru Mungu kwa kunipa kipaji hiki cha uimbaji na taaluma ya uuguzi na ukunga. Wengi huwa wanasema mshika mawili moja humponyoka, lakini kwangu ni heri kwani siamini kama nimeweza kwenda na muziki na masomo.” Alisema hantish. Pia aliongeza kuwa mbali na hayo yote aliyo yapata, ameweza kuandaa albam yenye nyimbo 8 kwa mchanganuo ufuatao;- 1. Nikupe nini mwili? 2. Asubuhi njema. 3. Tunakuabudu Bwana. 4. Iguse Tanzania. 5. Nimekukimbilia wewe. 6. Fanya hima niokoe. 7. Twaja mbele zako. 8. Siku yaja. 



ukoo wake hantish kwa upande wa mamayake
babu yake anaitwa Omary Juma mbakilwa, alioa mke wa kwanza aliyeitwa Bi. Ester Mchechumkulu ambaye alikua ni mtu wa Tanga kutoka katika kabila la wasambaa. Babu na bibi huyo walibahatika kuwa na mtoto mmoja aliyeitwa Christina mbakilwa ambaye ndiye aliyekuwa kifungua mimba na kitinda mimba pekee.  Kutoka na mazingira waliyokua wakiishi, babu aliamua kumwacha bibi ester na kumpata mke mwingine aliyeitwa Bi. Eliza Nyondo, mtu wa Malawi ambaye awali alitokea makete ukingani. Bibi huyo alijaliwa kumzalia babu watoto saba. 1. Asia 2. God 3. Joyce 4. Eliud 5. Anna 6. Agness 7. Alfa.
 Lakini kuna watoto aliobahatika kuwa nao babu kabla hajaingia  katika ndoa, ambao ni:- Jozack na mwezie ambaye alifariki. Daniel na Kelvin ni watoto aliowalea tangu baba yao ambaye ni                  mdogo wa omary mbakilwa{babu} afariki akiwaacha wadogo sana.